Sio kila mafanikio yanakuja kwa kufanya kazi kwa bidii. Na sio kila kufeli kuna sababishwa na uvivu.
Chuo kikuu cha dar es salaam kuna taasisi nyingi sana zinaongozwa na wanafunzi. Wakati mimi nipo chuo, miongoni mwa taasisi kubwa mbili zilikuwa ni AIESEC na DUFA, ambayo ilikuwa ni taasisi ya wanafunzi wa maswala ya fedha. Mwaka wangu wa pili nikiwa chuo nilipata uzoefu kwenye hizi taasisi. Nilipata ujuzi wa namna mambo yalivyokuwa yanaendeshwa.…
Vitu unavyomiliki vinabadilishika. Vitu usivyomiliki havibadilishiki.
Leo ni siku ya mwisho ya mwaka 2025. Sitengenezi malengo mapya ya mwaka unaofuata. Ninarudia kukagua na kupitia nini nilifanya mwaka huu. Na miongoni mwa vitu nilivyopitia ni vitu niliyopoteza, kuharibu au kuvunja. Vipo vingi sana. Nikiwa katikati ya kupitia nikakumbuka miaka mingi sana imepita na nimefanya kitu hiki sana. Kumbukumbu zikaanza kuja kuhusu vitu…
Vitu vyenye mafanikio vinachosha
Mara ya kwanza kupewa nafasi ya kuendesha gari ilikuwa na mjomba wangu, ambaye alikuwa ni dereva wa magari makubwa ya mizigo. Jioni moja alijitolea kunifundisha. Hiyo siku alirudi na daladala ndogo ambayo aliazima kwa rafiki yake kazini. Ilikuwa ni gari ya zamani na ilikuwa ni ya kubadilisha gia kwa mkono. Alinifundisha kwa masaa mawili na…
Kufanya kitu kisicho na maana vizuri hakukifanyi kiwe cha maana.
Nilipoanzisha kampuni yangu ya Emakatt, mazingira ya biashara changa za teknolojia yalikuwa yanaanza kuchangamka sana. Na nchini kwetu ilikuwa bado ni nadra sana kwa watu wengi kujihusisha hivyo ilikuwa rahisi sana kujuana. Ilikuwa kawaida kujiona kama sisi ni mashujaa na watu wenye uwezo mkubwa sana kwenye mazingira hayo. Ilikuwa haijalishi ndoto na malengo ambayo mtu…
Unadhani unapambana na dunia, lakini dunia haitambui hata uwepo wako
Utotoni sikuwahi kujiona nikiwa kiongozi kwenye ngazi yeyote ile. Na mara nyingi nilijitahidi kuepuka mazingira ya kuongoza au yaliyonihitaji kuwa mbele za watu. Sehemu pekee nilikuwa tayari kuwa mbele za watu ni wakati wa kucheza mpira wa miguu. Hali hiyo ilibadilika wakati najiunga sekondari ya Pugu Dar es Salaam. Rafiki yangu mmoja aligombea uongozi nafasi…
Watu wengi wanajikwaa kwenye vitu walivyopita na kuviacha nyuma.
Nilipoanza chuo kikuu niliweka lengo la kuwa na gari langu nikifika mwaka wa tatu. Ilikuwa ni ndoto yangu kununua Toyota Celica nyekundu au Altezza ya bluu. Nilifanikiwa kununua Toyota Celica nyekundu mwezi mmoja kabla ya mahafali ya chuo, ilikuwa ni kitu kikubwa sana maishani mwangu. Mara ya kwanza kumiliki kitu au kupitia kitu fulani huwa…
Usiamini sifa zako unazoweka kwenye mitandao ya jamii
Cheo kipi kizuri zaidi? Muanzilishi au Mkurugenzi? Nilikuwa nafikiria kitu gani cha kujaza kwenye wasifu wangu wa mtandao wa jamii wa LinkedIn. Kama ambavyo kila mtu hufanya, anaenda kwenye mitandao ya jamii hususani LinkedIn kutangaza sifa zake za kazi au biashara. Nilikuwa nimetoka kufanya kazi kama mkaguzi kwenye kampuni ya kimataifa, PwC Tanzania. Nilifanya mafunzo…
Kupata zaidi inabidi uwe wa ziada
Les Brown, mwandishi wa vitabu, mzungumzaji na mfanyabiashara wa Marekani aliwahi kusema, “Mafanikio sio kitu unachokipata, mafanikio ni mtu unayekuwa.” Haupati mafanikio, unakuwa mtu mwenye mafanikio. Watu wengi hawajaweza kujua utofauti, na ndio sababu ya kushindwa kupanda kwenye ngazi ya mafanikio. Baada ya muda, vitu vizuri huja kwetu sote, lakini vinakuja haraka sana kwa wale…
Kila kitu kina gharama yake, lakini sio kila gharama inaonekana.
Mwaka jana, madaktari walinipima na kuniambia kuwa nina bakteria wanaoitwa H.pylori wanaosababisha vidonda vya tumbo. Bakteria hawa walikuwa wanakula kuta za utumbo na kusababisha vidonda. Mara nyingi ndio sababu kubwa sana ya watu kupata vidonda vya tumbo au hata kansa ya tumbo. Kabla ya siku hii, sikuwahi kusikia neno H.pylori kwenye maisha yangu. Maumivu niliyokuwa…
Wapishi wazuri wanajua kiwango sahihi cha chumvi
Kukua kwangu kote nimezungukwa na wanawake. Na sio tu wanawake wa kawaida, bali wale waliopenda na kujua sana kupika. Bibi yangu alikuwa anafanya biashara ya vitumbua kwa maisha yangu yote niliyomjua. Nakumbuka wakati wa likizo sisi wajukuu ndio tulikuwa wauzaji wake. Mama yangu ni miongoni mwa wapishi wangu bora kabisa duniani. Na hii ni kitu…
Kama unahitaji kuhamasishwa kuanza jambo, basi umeshafeli.
Zamani nilikuwa natafuta njia zozote za kupata hamasa kwenye maisha. Kutokea kwenye familia ya kipato cha chini, kuzungukwa na umasikini na ndugu wasio na kipato ilikuwa inakatisha tamaa. Kila nilipopata hamasa au moyo kidogo nilikuwa naona maisha kwa jicho la utofauti. Nikaanza kuwa mpenzi mkubwa sana wa vitu vyote vilivyogusa masuala ya hamasa, mawazo chanya…
