Vitu viwili vinagusa kila mtu: fedha na afya
Wiki iliyopita nilisimulia kuhusu stori ya bibi yangu. Alifariki miaka michache nyuma akiwa na miaka mia moja na tatu, miaka nadra sana kwa watu kuishi kwa kizazi hiki. Miezi kadhaa kabla ya kifo chake, bibi alikuwa amepooza mwili wote upande wa kushoto. Alikuwa hawezi kutembea wala kufanya shughuli za kila siku za kujitunza. Alikuwa anategemea…
Nini thamani ya mali bila kuwa na furaha?
Bibi yangu mzaa baba alifariki miaka michache iliyopita akiwa na miaka mia moja na tatu. Mwaka mmoja kabla ya kifo chake alikuwa amepata mshituko na kupooza upande wake wa kushoto. Hivyo alikuwa hawezi kutembea, muda wote yupo ndani. Wiki moja kabla ya kupata mshtuko na kupooza alitoka kushinda kesi mahakamani. Kesi ilikuwa inahusu viwanja ambavyo…
Hakuna kitu kinachoitwa mwisho mzuri.
Nilianza kusoma darasa la kwanza kwenye shule ya msingi ambayo ilikuwa imeanzishwa mwaka mmoja nyuma. Darasa letu lilikuwa ndio la pili kujiunga na shule, hivyo tulikuwa tunapewa uangalizi wa utofauti sana. Darasani tulikuwa watu ishirini na sita, watatu wakiwa ni wasichana na wengine wote walikuwa wavulana. Miaka kadhaa mbele waliongezeka wasichana wawili na wavulana wawili. …
Kinachoonekana cha ajabu au kijinga kwako ni cha kawaida na kueleweka kwa wengine.
Nina mdogo wangu mmoja ambaye anapenda sana michezo ya kukimbiza magari na kutelezesha matairi ya gari kwenye lami. Hutumia muda mwingi na fedha nyingi sana kwenye gari lake. Huwa anaangalia kila aina ya video yenye kuonyesha watu wakifanya kama yeye pia. Mwanzoni nilikuwa naona ni kitu cha ajabu sana. Nina rafiki mmoja ambaye anapenda sana…
Sio kila mafanikio yanakuja kwa kufanya kazi kwa bidii. Na sio kila kufeli kuna sababishwa na uvivu.
Chuo kikuu cha dar es salaam kuna taasisi nyingi sana zinaongozwa na wanafunzi. Wakati mimi nipo chuo, miongoni mwa taasisi kubwa mbili zilikuwa ni AIESEC na DUFA, ambayo ilikuwa ni taasisi ya wanafunzi wa maswala ya fedha. Mwaka wangu wa pili nikiwa chuo nilipata uzoefu kwenye hizi taasisi. Nilipata ujuzi wa namna mambo yalivyokuwa yanaendeshwa.…
Vitu unavyomiliki vinabadilishika. Vitu usivyomiliki havibadilishiki.
Leo ni siku ya mwisho ya mwaka 2025. Sitengenezi malengo mapya ya mwaka unaofuata. Ninarudia kukagua na kupitia nini nilifanya mwaka huu. Na miongoni mwa vitu nilivyopitia ni vitu niliyopoteza, kuharibu au kuvunja. Vipo vingi sana. Nikiwa katikati ya kupitia nikakumbuka miaka mingi sana imepita na nimefanya kitu hiki sana. Kumbukumbu zikaanza kuja kuhusu vitu…
Vitu vyenye mafanikio vinachosha
Mara ya kwanza kupewa nafasi ya kuendesha gari ilikuwa na mjomba wangu, ambaye alikuwa ni dereva wa magari makubwa ya mizigo. Jioni moja alijitolea kunifundisha. Hiyo siku alirudi na daladala ndogo ambayo aliazima kwa rafiki yake kazini. Ilikuwa ni gari ya zamani na ilikuwa ni ya kubadilisha gia kwa mkono. Alinifundisha kwa masaa mawili na…
Kufanya kitu kisicho na maana vizuri hakukifanyi kiwe cha maana.
Nilipoanzisha kampuni yangu ya Emakatt, mazingira ya biashara changa za teknolojia yalikuwa yanaanza kuchangamka sana. Na nchini kwetu ilikuwa bado ni nadra sana kwa watu wengi kujihusisha hivyo ilikuwa rahisi sana kujuana. Ilikuwa kawaida kujiona kama sisi ni mashujaa na watu wenye uwezo mkubwa sana kwenye mazingira hayo. Ilikuwa haijalishi ndoto na malengo ambayo mtu…
Unadhani unapambana na dunia, lakini dunia haitambui hata uwepo wako
Utotoni sikuwahi kujiona nikiwa kiongozi kwenye ngazi yeyote ile. Na mara nyingi nilijitahidi kuepuka mazingira ya kuongoza au yaliyonihitaji kuwa mbele za watu. Sehemu pekee nilikuwa tayari kuwa mbele za watu ni wakati wa kucheza mpira wa miguu. Hali hiyo ilibadilika wakati najiunga sekondari ya Pugu Dar es Salaam. Rafiki yangu mmoja aligombea uongozi nafasi…
Watu wengi wanajikwaa kwenye vitu walivyopita na kuviacha nyuma.
Nilipoanza chuo kikuu niliweka lengo la kuwa na gari langu nikifika mwaka wa tatu. Ilikuwa ni ndoto yangu kununua Toyota Celica nyekundu au Altezza ya bluu. Nilifanikiwa kununua Toyota Celica nyekundu mwezi mmoja kabla ya mahafali ya chuo, ilikuwa ni kitu kikubwa sana maishani mwangu. Mara ya kwanza kumiliki kitu au kupitia kitu fulani huwa…
Usiamini sifa zako unazoweka kwenye mitandao ya jamii
Cheo kipi kizuri zaidi? Muanzilishi au Mkurugenzi? Nilikuwa nafikiria kitu gani cha kujaza kwenye wasifu wangu wa mtandao wa jamii wa LinkedIn. Kama ambavyo kila mtu hufanya, anaenda kwenye mitandao ya jamii hususani LinkedIn kutangaza sifa zake za kazi au biashara. Nilikuwa nimetoka kufanya kazi kama mkaguzi kwenye kampuni ya kimataifa, PwC Tanzania. Nilifanya mafunzo…
